Shahidi asimulia kilichojiri nyumbani kwa Tob Cohen kabla ya kifo chake
Description (show more)
Aliyekuwa mfanyakazi wa nyumbani wa marehemu Tob Cohen, ameieleza mahakama kuhusu kile alichodai ni kushuhudia yaliyokuwa yakijiri nyumbani kwa Cohen mnamo tarehe 8 Februari 2018 siku kumi kabla ya mauaji yake. Shilindwa Shishemi amesema alimsikia Cohen akipiga kelele kabla ya kutoka nje na kumkuta akiwa ameanguka chini huku mkewe Sarah akiwa amemfinya sakafuni kwa kutumia kiti. Kisa ambacho kilisababisha Cohen kujeruhiwa na kutoka damu kichwani. Shahidi huyo pia alielezea kuhusu mivutano kati ya Cohen na Sarah, akisema wawili hao walikuwa wameacha kuzungumza na hata kuandaa chakula tofauti. Shishemi aliarifu mahakama kuwa baada ya Cohen kutoweka, Sarah alimwambia kwamba alikuwa amesafiri nje ya nchi kwa matibabu. Ushahidi wake ni sehemu ya kesi ambayo mahakama inasikiliza ili kubaini kutoweka kwa Tob Cohen na kisha kifo chake.
Related Videos
More from Citizen TV Kenya
28:31🔴LIVE || VUTA STOOL || TV47KENYA
46:55Curbing Road Accidents: What Kenya Must Do | Dr Duncan Kibogong
25:37National Leaders or Tribal Politicians? || TV47 Breakfast || 04.11.2026
1:59Odede: Gachagua’s numbers game sidelines smaller parties in Opposition power-sharing talks
3:52Gitau: Gachagua: Numbers will determine who shapes the next government!
44:25🔴LIVE || MEZESHA || TV47KENYA
4:05Advice: Gachagua is dragging Opposition leaders into his ethnic numbers game
2:03:21