Kenyans Live

Nyoro ampa Ruto siku 14 kuweka wazi mkataba wa mradi wa Dangote Lamu

Description (show more)

Kinara wa People’s Party of Kenya, Ndindi Nyoro, amempa Rais William Ruto siku 14 kuweka wazi mkataba wa makubaliano kati ya serikali na mwekezaji Aliko Dangote kuhusu ujenzi wa kiwanda cha kusafishia mafuta mjini Lamu. Nyoro pia ametaka kuwekwa wazi orodha ya wanahisa wa kampuni ya Dangote East Africa Refinery, akisema Wakenya wana haki ya kufahamu muundo wa umiliki wa mradi huo. Nyoro amesema madai hayo yanalenga kuongeza uwazi kuhusu mradi huo, ambao unakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi trilioni mbili. Haya yanajiri huku Naibu Kinara wa Jubilee, Fred Matiang’i, akiendelea na ziara yake ya siku tano katika ukanda wa Pwani. Matiang’i ameitaka serikali kuchunguza na kuwachukulia hatua waliohusika na kusitishwa kwa mradi wa kiwanda cha saruji katika serikali iliyopita, akisema suala hilo lisitumike kumlaumu Rais mstaafu Uhuru Kenyatta.

Share: