Kenyans Live

Matamshi ya Joho kuhusu uvuvi Ziwa Nakuru yazua utata

Description (show more)

Utata umeibuka kuhusu shughuli za uvuvi katika Ziwa Nakuru kufuatia matamshi ya Waziri wa Madini na Uchumi wa Bahari, Hassan Joho, aliyeripotiwa kuunga mkono shughuli hiyo na kuwaagiza polisi kutowakamata wavuvi. Matamshi hayo aliyotoa mjini Nakuru yamezua mjadala kuhusu uhalali wa biashara hiyo, ambayo imeendelea kwa miaka kadhaa licha ya maonyo ya mara kwa mara kuwa ni haramu. Sasa maswali yanaibuka kuhusu msimamo wa serikali kuhusu uvuvi katika ziwa hilo na hatua zitakazochukuliwa kudhibiti shughuli hiyo. Maryanne Nyambura anaripoti.

Share: