Kenyans Live

Watu watatu waangamia Lari, Kiambu baada ya kubugia pombe haramu

Description (show more)

Watu watatu wamefariki na wengine kadhaa wamelazwa wakiwa mahututi katika vituo mbali mbali vya afya katika eneo bunge la Lari, kaunti ya Kiambu baada ya kunywa inayodaiwa kuwa pombe haramu mjinin Kimende. Wakazi wa Kimende walioghadhabika walivamia baa moja inayoshukiwa kuwauzia waathiriwa pombe hiyo yenye sumu, huku kitengo cha maafisa wa idara mbali mbali kikianzisha uchunguzi kuhusu kisa hicho. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive

Share: