Kenyans Live

Kampuni ya KenGen yawataka wakazi karibu na mabwawa ya Mto Tana kuhamia maeneo salama

Description (show more)

Kampuni ya kuzalisha umeme ya KenGen imewataka wakazi na wakulima wanaoishi karibu na mabwawa yake katika mto Tana kuhamia maeneo salama, huku mvua kubwa inayoendelea kunyesha ikitarajiwa kuongeza viwango vya maji na kuhatarisha jamii zinazoishi maeneo ya chini ya mkondo wa maji . KenGen inasema inaendelea kufuatilia hali ya mabwawa yake na kuchukua hatua za tahadhari kudhibiti ongezeko la maji na kuzuia maafa.

Share: