Kenyans Live

Waziri wa kawi Opiyo Wandayi akosoa upinzani kuhusu miradi ya maendeleo

Description (show more)

Waziri wa kawi Opiyo Wandayi, amekosoa vikali upinzani kwa kile alichokitaja kuwa hulka ya kupinga miradi ya maendeleo. Akizungumza baada ya kukagua eneo la kumbukunbu la Raila Odinga, waziri huyo alisema kuwa nakala za ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta ghafi cha Dangote zipo katika wizara ya kawi na kuwa yupo tayari kutoa maelezo kuhusu kiwanda hicho. Aidha alisema kuwa serikali inakamilisha mipango ya ujenzi wa kituo cha nukliya eneo la Lenya kaunti ya Siaya, ikiwa moja kati ya mpango wa kukuza viwanda, kutoa nafasi za ajira na kuimarisha uchumi kwa jumla

Share: