Kenyans Live

Kenya Kwanza yamshinikiza Uhuru ajitenge na siasa

Description (show more)

Wanasiasa wa Kenya Kwanza, wakiongozwa na Spika wa Bunge la Kitaifa, Moses Wetang’ula, wameendeleza ukosoaji wao dhidi ya rais mstaafu Uhuru Kenyatta, wakimtuhumu kuendeleza upinzani dhidi ya serikali ya Rais William Ruto. Viongozi hao wamemtaka Uhuru kujiepusha na siasa za sasa, wakisema anafaa kuheshimu nafasi yake kama rais mstaafu na kuepuka shughuli wanazodai zinadhoofisha hadhi ya wadhifa huo. Wetang’ula na washirika wengine wa Kenya Kwanza wameendelea kumkosoa Uhuru huku nchi ikielekea uchaguzi mkuu wa 2027. Bonface Barasa na mengi zaidi.

Share: