Kenyans Live

Wanaharakati wawili hawajulikani walipo baada ya maandamano ya Besigye

Description (show more)

Wanaharakati wawili nchini sasa hawajulikani walipo katika matukio mawili tofauti baada ya kushiriki maandamano ya kutaka kuachiliwa kwa mwanasiasa wa upinzani wa Uganda, Kizza Besigye. Muling'e Muteti amekuwa akitafutwa kwa saa 72 sasa, huku Collins Otieno akitoweka siku moja tu baada ya kuachiliwa. Familia pamoja na mawakili wamewasilisha ombi mahakamani wakitaka serikali ilazimishwe kumfikisha Muteti mahakamani.

Share: