Kenyans Live

Viongozi wa DCP wamtaka Ruto kukubali kushindwa uchaguzi ujao

Description (show more)

Katibu Mkuu wa chama cha DCP, John Methu, ameongoza viongozi wa chama hicho kumkosoa Rais William Ruto, wakidai ameshindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Wakizungumza katika mkutano wa hadhara eneo la Githogoro, kaunti ya Kiambu, viongozi hao wamewataka Wakenya kumpigia kura mgombea mwingine katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao. Wamesema hatua hiyo ni muhimu katika kuleta mabadiliko ya uongozi nchini, huku wakikosoa utendakazi wa serikali ya Rais Ruto.

Share: