Kenyans Live

Maafisa wawili wa polisi kuzuiliwa hadi Oktoba 27 kwa mauaji ya wakili Mbobu

Description (show more)

Maafisa wawili wa polisi ambao ni washukiwa wa mauaji ya wakili Mathew Kyalo Mbobu watasalia katika rumande ya Industrial Area hadi tarehe 27 mwezi huu, ambapo watasomewa mashtaka. Washukiwa hao watafikishwa katika Hospitali ya Mbagathi kwa uchunguzi wa afya ya akili. Julius Kipkoech Cheruiyot na Kennedy Kipkemei Borboroi sasa wanakabiliwa na mashtaka ya kumuua wakili Mbobu tarehe 9 Septemba 2025 katika barabara ya Magadi-Rongai. Wanatarajiwa kushtakiwa pamoja na Rose Mbithe, Chris Mulwa na Angela Mulwa, ambao wanahusishwa na mauaji ya Dkt. Victoria Mutiso.

Share: