Kenyans Live

Upinzani waipongeza mahakama kwa kubatilisha uuzaji wa hisa za Safaricom

Description (show more)

Muungano wa upinzani, ukiongozwa na kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka, umepongeza uamuzi wa Mahakama Kuu wa kubatilisha uuzaji wa hisa zinazomilikiwa na serikali katika kampuni ya Safaricom. Upinzani sasa unaitaka serikali kuheshimu uamuzi wa mahakama na kurejesha fedha ilizopokea, ukisema hautakubali uuzaji wa hisa hizo kwa kuwa Safaricom inatekeleza majukumu muhimu nchini, ikiwemo katika uchaguzi mkuu ujao.

Share: