Kenyans Live

Radio Citizen yawafikia wasikilizaji wake Kitengela

Description (show more)

Watangazaji wa Radio Citizen wamezuru Kitengela, kaunti ya Kajiado, kwa ibada ya Jumapili katika kanisa la Glorious Gospel Centre. Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za Radio Citizen kuwafikia wasikilizaji wake moja kwa moja na kuimarisha uhusiano na mashabiki wake kote nchini. Askofu wa GCC, Bonface Mangeti, amesisitiza umuhimu wa vyombo vya habari katika kuunganisha jamii, akitambua mchango wa Radio Citizen kupitia vipindi vyake. Royal Media Services imezidisha uwepo wake mashinani kwa lengo la kuwafikia na kuwashirikisha wasikilizaji wa vituo vyake.

Share: