Kenyans Live

Gachagua akosoa serikali kwa madai ya kuandaa wizi wa kura

Description (show more)

Kinara wa DCP, Rigathi Gachagua, ameendelea kuikosoa serikali ya Rais William Ruto, akidai kuna njama ya kuiba kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao. Akizungumza nchini Marekani wakati wa kikao na Wakenya, Gachagua alidai kuwa kuna mipango ya kuwasajili raia wa nchi jirani ya Uganda pamoja na kutumia majina ya watu waliofariki ili kumsaidia Rais Ruto kusalia mamlakani. Hata hivyo, madai ya usajili wa raia wa kigeni yamekanushwa na IEBC, ambayo imesema haijapokea ushahidi wa kuaminika kuhusu usajili haramu wa wageni kama wapiga kura. Gachagua pia amedai kuwa umaarufu wa Rais Ruto unaendelea kudidimia, akisema hali hiyo imemfanya rais kuanza kubabaika. Ben Kirui ana taarifa zaidi.

Share: