Kenyans Live

Karua, Nyoro wataka umoja wa upinzani

Description (show more)

Kinara wa chama cha PLP Martha Karua na mwenzake wa People's Party Ndindi Nyoro wamewataka viongozi wenzao wa upinzani kusitisha malumbano na kumkaribisha kila kiongozi anayetaka kujiunga na mrengo huo ili kumng’oa Rais William Ruto mamlakani. Akizungumza huko Kipipiri, Kaunti ya Nyandarua, Karua amewataka wanaojiunga na upinzani kutowekewa masharti, huku Nyoro akimtetea Rais mstaafu Uhuru Kenyatta na kushinikiza umoja miongoni mwa viongozi wa upinzani.

Share: