Kenyans Live

Mahakama yaamuru kurejeshwa kwa marupurupu ya Uhuru Kenyatta

Description (show more)

Imekuwa afueni kwa Rais mstaafu Uhuru Kenyatta baada ya Mahakama Kuu kuamua kuwa kuzuiwa kwa baadhi ya marupurupu yake ni kinyume na katiba. Akibatilisha baadhi ya vifungu vya Sheria ya Marupurupu ya Marais Wastaafu, Jaji Bahati Mwamuye amesema vifungu hivyo haviwezi kutumiwa kupunguza, kunyima, kuzuia ama kuondoa marupurupu anayostahili kupewa rais anapostaafu. Mahakama pia imebatilisha Kifungu cha 6 cha sheria hiyo, kilichokuwa kinaweka vikwazo kwa rais mstaafu kushiriki kikamilifu katika siasa.

Share: