Kenyans Live

Mvutano wazidi kuhusu soko la Masinde Muliro Kitale

Description (show more)

Hali ya taharuki na ulinzi mkali ilitanda katika mji wa Kitale, kaunti ya Trans Nzoia, kufuatia mvutano kuhusu soko la Masinde Muliro, ambapo Gavana George Natembeya alitarajiwa kuongoza maombi. Mvutano kuhusu soko hilo kati ya Rais William Ruto na Gavana Natembeya ulionekana kushamiri leo, huku juhudi za kuandaa maombi katika ofisi za kaunti pia zikikwama. Hali hiyo imezua maswali kuhusu mustakabali wa soko hilo huku mvutano kati ya viongozi hao ukiendelea. Collins Shitiabayi anaripoti.

Share: