Kenyans Live

Operesheni za kutafuta na kuokoa watu walioangukiwa na jengo Eastleigh zimeingia siku ya nne

Description (show more)

Operesheni za kutafuta na kuokoa watu walioangukiwa na jengo Eastleigh zimeingia siku ya nne Jumatatu, matumaini ya kuwapata wakiwa hai yakididimia kila dakika. Familia zimezidi kukesha zikielekeza macho yao kwenye eneo la mkasa ambapo vikosi vya uokoaji na majanga vinaendelea kuchimbua vifusi. Watu wawili tu wamefanikiwa kuokolewa hadi sasa. Wawili hao walitolewa wakiwa hai Jumamosi. Watu 47 wanahofiwa kukwama ndani ya vifusi.

Share: