Kenyans Live

Royal Media Services yatuzwa kwa uongozi bora na ubora wa huduma

Description (show more)

Kampuni ya habari ya Royal Media Services imepokea tuzo ya uongozi bora kimataifa kwa utendakazi wake na ukakamavu wa huduma zake nchini. Royal Media Services imepokea tuzo hiyo wakati wa hafla ya utoaji wa shahada za uzamili iliyoandaliwa na chuo cha kimataifa cha United Graduate College and Seminary International (UGSCI) katika Chuo Kikuu cha Daystar. Ak ipokea tuzo hiyo kwa niaba ya Royal Media, mwanahabari nguli Fred Obachi Machoka alitunukiwa tuzo ya ubalozi kwa kutambua zaidi ya miaka hamsini ya mchango na umahiri wake katika tasnia ya uanahabari.

Share: