Kenyans Live

Afisa wa kaunti auaawa katika shambulizi la Likoni, Mombasa

Description (show more)

Afisa mmoja wa kaunti ameuawa huku wengine watatu wakijeruhiwa, akiwemo afisa wa polisi, baada ya kuvamiwa na genge la wahalifu waliokuwa na silaha katika kituo cha kukusanya ushuru wa kaunti eneo la Likoni, Mombasa. Genge hilo limetoroka na bunduki huku maafisa wa polisi wakianzisha uchunguzi kuhusu shambulizi hilo lililotokea alfajiri ya leo. Francis Mtalaki anaripoti kutoka Mombasa.

Share: