Kenyans Live

Utata wa soko la Masinde Muliro wazua maswali kuhusu matumizi ya fedha

Description (show more)

Mvutano kuhusu soko la Masinde Muliro mjini Kitale, kaunti ya Trans Nzoia, umeendeleza mzozo kati ya Rais William Ruto na Gavana wa kaunti hiyo, George Natembeya. Serikali ya kaunti inasema imetumia shilingi milioni 821 katika mradi huo, huku serikali ya kitaifa ikidai kuwa ilitumia shilingi milioni 100 kupitia mpango wa ukarabati wa masoko. Tofauti hiyo ya madai kuhusu fedha zilizotumika imeibua maswali kuhusu ufadhili wa mradi huo, utekelezaji wake na uwajibikaji katika matumizi ya fedha za umma. Willy Lusige anatathmini historia ya mradi huo na maswali yanayoibuka kuhusu gharama ya ujenzi wa soko hilo.

Share: