Kenyans Live

Wabunge wa kike wa Kenya Kwanza wampigia debe Ruto 2027, wataka upinzani kuzingatia maendeleo

Description (show more)

Vuguvugu la wabunge wa kike wanaounga mkono serikali ya Kenya Kwanza limeendeleza kampeni za kumpigia debe Rais William Ruto kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027, wakisema anapaswa kupewa fursa ya kukamilisha miradi ya maendeleo nchini. Wabunge hao, waliozungumza katika hafla ya kuchangisha fedha na kuimarisha makundi ya kina mama katika eneo la Sendera, eneo bunge la Endebess, kaunti ya Trans Nzoia, pia wamewataka wanasiasa wa upinzani kuzingatia ajenda za maendeleo badala ya matamshi wanayosema yanaweza kuchochea Wakenya.

Share: