Kenyans Live

Mackenzie apatikana na hatia ya mauaji ya Shakahola

Description (show more)

Mahakama Kuu ya Mombasa imempata na hatia mhubiri Paul Nthenge Mackenzie na wenzake 28 kuhusiana na vifo vya waumini katika msitu wa Shakahola, kaunti ya Kilifi. Jaji Diana Kavedza ameamua kuwa washtakiwa hao wana hatia ya kuwapotosha waumini, hali iliyosababisha vifo vya baadhi yao kati ya mwaka 2021 na 2023. Mackenzie na wenzake walipatikana na hatia kufuatia mashtaka 191 ya mauaji. Mahakama inatarajiwa kutoa hukumu dhidi ya washtakiwa hao tarehe sita Novemba.

Share: