Kenyans Live

Watu 47 hawajulikani walipo baada ya jengo kuporomoka Eastleigh

Description (show more)

Operesheni ya kutafuta watu walionasa kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka mtaani Eastleigh, jijini Nairobi, imeingia siku ya tatu leo, huku waokoaji wakikosa kuwafikia waathiriwa wowote kutwa nzima. Familia za waathiriwa zimeendelea kukesha na kutumia muda wao katika eneo la mkasa, zikishikilia matumaini kuwa jamaa zao watapatikana salama. Haya yanajiri huku Shirika la Msalaba Mwekundu likiripoti kuwa watu 47 wameripotiwa kutoweka, kama Ben Kirui anavyotuarifu.

Share: