Kenyans Live

Ruto atangaza msamaha wa ushuru kwa wanaopata chini ya Sh32,333

Description (show more)

Rais William Ruto ametangaza kuwa Wakenya wanaopokea mshahara wa chini ya shilingi 32,333 kwa mwezi wataondolewa ushuru wa mapato, katika juhudi za kuongeza kipato kinachobaki mikononi mwao. Akizungumza wakati wa sherehe za 63 za Mashujaa zilizofanyika katika kaunti ya Uasin Gishu, Rais Ruto pia alitangaza kuondolewa kwa ushuru wa asilimia 25 wa simu, akisema serikali yake inalenga kupunguza zaidi gharama ya maisha kwa Wakenya. Emmanuel Too anatueleza zaidi.

Share: