Kenyans Live

Wakazi wa Magogoni wataka ardhi mbadala kwa mradi wa Dangote

Description (show more)

Maelfu ya wakazi wa eneo la Magogoni, Kaunti ya Lamu, sasa wanaitaka serikali kuwapa sehemu mbadala ya kuishi ili kupisha ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta ghafi cha Dangote. Baadhi ya wakazi hao wamekiri kutokuwa na hati miliki za vipande vya ardhi wanavyoishi, licha ya kusema wameishi katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka 20. Ombi hilo linajiri baada ya Rais William Ruto kusema kuwa serikali haitawafidia maskwota wanaoishi kwenye ardhi ya serikali. Wakati huo huo, Waziri John Mbadi amewalaumu baadhi ya mabwenyenye kwa kuwachochea wakazi kupinga mradi huo.

Share: