Kenyans Live

Ruto atangaza vita dhidi ya matapeli wanaowahangaisha wawekezaji

Description (show more)

Rais William Ruto amesema atakabiliana vikali na matapeli wanaowahangaisha wawekezaji nchini, akilaumu urasimu na rushwa kwa kuchelewesha au kukwamisha miradi inayoweza kuwanufaisha Wakenya. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa kampuni ya saruji katika Kaunti ya Kitui, Rais Ruto ameamuru kampuni nne mpya kuruhusiwa kuendesha biashara ya magadi nchini ili kuvunja ukiritimba wa kampuni ya Tata Chemicals. Kama anavyoripoti Emmanuel Too, Rais amemtaka Waziri wa Madini kutekeleza agizo hilo, akisema hatua hiyo itasaidia Kenya kuacha kuuza nje magadi ghafi.

Share: