Kenyans Live

Watu 10 watengwa kwa uchunguzi wa Ebola, Serikali yafuatilia wengine 57

Description (show more)

Watu kumi wametengwa kwa uchunguzi wa maambukizi ya Ebola baada ya kutangamana na mgonjwa aliyefariki Jumatatu, huku Serikali ikiendelea kuwafuatilia watu wengine 57 waliokuwa wamewasiliana na mgonjwa huyo. Haya yanajiri huku Wizara ya Afya ikiimarisha uchunguzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) kwa wasafiri wanaotoka katika mataifa yanayopakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na yaliyo katika hatari ya Ebola. Kama anavyoripoti Ben Kirui, vituo vitano vya afya vimetengwa kuwahudumia watu wanaoshukiwa kuambukizwa virusi vya Ebola.

Share: