Kenyans Live

Kijana wa Gen Z asubiri haki miaka miwili baada ya kupigwa risasi

Description (show more)

Miaka miwili baada ya maandamano ya vijana wa kizazi cha Gen Z kupinga Mswada wa Fedha, kijana mmoja bado anasubiri fidia baada ya kupigwa risasi tatu zilizompokonya uwezo wa kutembea. Ian Keya, aliyekuwa mwanafunzi na mtaalamu wa lishe, alipigwa risasi kwenye uti wa mgongo, hali iliyomfanya sasa kutegemea kiti cha magurudumu. Kama anavyoarifu Brenda Wanga, Ian anasikitikia mabadiliko makubwa katika mkondo wa maisha yake huku akiendelea kusubiri haki.

Share: