Kenyans Live

Wahudumu wa afya watishia kusitisha huduma wakidai hawajaandaliwa kukabiliana na Ebola

Description (show more)

Miungano ya wahudumu wa afya ya umma imetishia kusitisha huduma zao kote nchini, ikilalamikia Wizara ya Afya kwa kile inachodai ni kuwahadaa Wakenya kuhusu kiwango cha maandalizi ya kukabiliana na virusi vya Ebola. Wahudumu hao wanasema hawajapewa mafunzo ya kutosha wala vifaa vya kujikinga, licha ya kuwa miongoni mwa walio katika hatari kubwa ya kuambukizwa wakati wa kuwahudumia wagonjwa.

Share: