Kenyans Live

Ruto awataka walimu kuimarisha maandalizi na uadilifu wa mitihani

Description (show more)

Rais William Ruto amewataka walimu kuhakikisha watahiniwa wanaandaliwa vilivyo kwa ajili ya mitihani ya kitaifa inayokaribia, huku wakizingatia uadilifu katika mitihani hiyo. Akizungumza wakati wa sherehe za Siku ya Walimu Duniani katika Uwanja wa Kasarani jijini Nairobi, Rais Ruto alionya dhidi ya udanganyifu katika mitihani, akisema unaweza kudhoofisha thamani ya vyeti vya masomo. Aidha, Rais Ruto ameagiza Tume ya Huduma za Walimu, TSC, kuongeza nafasi za ajira na vyeo kwa walimu kutoka 34,000 hadi 50,000 katika mwaka wa kifedha wa 2026/27. Kwa upande wake, Waziri wa Elimu Julius Ogamba amewataka wahadhiri wa vyuo vikuu wanaogoma kurejea kazini kwa mujibu wa amri ya mahakama.

Share: