Kenyans Live

Harusi ya Februari yageuka msiba baada ya mpenzi kuangamia katika ajali

Description (show more)

Mmoja wa walioangamia katika ajali ya barabarani iliyotokea Salama, wakielekea Subukia, alikuwa amepanga kufunga ndoa na mpenzi wake mwezi Februari mwaka ujao. Leonea Baraza sasa ameachwa na simanzi baada ya mpenzi wake, Veronicah Ngandi, kuangamia katika ajali hiyo. Wawili hao walikuwa wamekamilisha taratibu za kulipa mahari mwezi Agosti, huku wakijiandaa kuanza maisha ya ndoa. Kwa masikitiko, Baraza alizungumza na mpenzi wake muda mfupi tu kabla ya ajali hiyo kutokea. Mipango ya harusi sasa imegeuka kuwa majonzi, huku familia na marafiki wakiomboleza kifo cha Veronicah.

Share: