Kenyans Live

Kanja: Polisi wamejiandaa kukabiliana na ghasia wakati wa uchaguzi

Description (show more)

Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja amesema maafisa wa polisi wamejiandaa vilivyo kukabiliana na rabsha au ghasia zozote wakati wa uchaguzi. Akizungumza katika shule ya mafunzo ya polisi jijini Nairobi, Kanja amewaonya wanasiasa dhidi ya kushirikiana na wahuni, akisema polisi wako macho kukabiliana na visa vyovyote vya magenge ya wahuni. Inspekta Jenerali huyo amesema polisi watadumisha usalama kwa kuzingatia sheria.

Share: