Kenyans Live

Polisi Kitale wakamata washukiwa 61 kufuatia mapigano ya magenge

Description (show more)

Polisi mjini Kitale wamewakamata washukiwa 61 kufuatia visa vya utovu wa usalama vilivyosababishwa na uhasama baina ya makundi mawili ya magenge katika mitaa ya Premium na Shanti, viungani mwa mji wa Kitale. Msako huo unajiri baada ya wakazi wa maeneo hayo kulalamikia usalama wao, suala lililowalazimu kufunga biashara zao mapema huku wengine wakihama.

Share: