Kenyans Live

Ruto adai serikali yake imeunda ajira milioni mbili

Description (show more)

Rais William Ruto anasema serikali yake imebuni nafasi milioni mbili za ajira tangu mwaka wa 2022, akidai kuwa Wakenya sasa wana fedha zaidi mifukoni. Akizungumza mjini Eldoret, kaunti ya Uasin Gishu, leo, Rais Ruto alikutana na wazee kutoka jamii ya Kalenjin na kuendelea kutetea ajenda yake ya usawa kwa wote. Rais huyo amesema serikali yake imepunguza pengo kati ya matajiri na maskini nchini, akisisitiza kuwa sera zake za kiuchumi zinaimarisha hali ya maisha ya Wakenya. Hata hivyo, madai hayo kuhusu ajira na hali ya kiuchumi yanaendelea kuwa sehemu ya mjadala kuhusu utendaji wa serikali yake.

Share: