Kenyans Live

Mamlaka ya usambazaji wa dawa KEMSA yataka kaunti kuidhinisha malipo ya dawa kupitia SHA

Description (show more)

Mamlaka ya usambazaji wa dawa imezitaka serikali za kaunti nchini kutia saini makubaliano ya pamoja na mamlaka ya afya ya jamii, sha pamoja na vituo vya afya, ili kuruhusu malipo ya kemsa kufanywa moja kwa moja kutoka kwa sha. Hatua hiyo inalenga kukabiliana na upungufu wa dawa katika vituo vya afya vya kaunti pamoja na madeni yanayodaiwa na kemsa. Mamlaka hiyo imeeleza kuwa mfumo huo umefaulu katika hospitali saba za rufaa nchini.

Share: