Kenyans Live

Wakazi wa Kajiado wataka hatua za haraka kukomesha mauaji ya wanawake

Description (show more)

Polisi katika Kaunti ya Kajiado wametakiwa kuimarisha uchunguzi na kuchukua hatua za haraka kuzuia ongezeko la visa vya mauaji ya wanawake. Wakizungumza wakati wa mazishi ya Catherine Mbithe, mwanamke aliyeuawa kwa kudungwa kisu, yaliyofanyika katika eneo la Mukaa, Kaunti ya Makueni, wakazi wa Kajiado wanasema licha ya ongezeko la mauaji ya wanawake, wahusika wengi hawajatiwa mbaroni wala kufunguliwa mashtaka.

Share: