Kenyans Live

Naibu rais Kithure Kindiki aahidi miradi ya maendeleo Laikipia baada ya kuimarika kwa usalama

Description (show more)

Naibu wa rais kithure kindiki amesema serikali itawekeza katika miradi ya maendeleo ili kuboresha uchumi wa maeneo yaliyoathirika hapo awali kutokana na utovu wa usalama uliochangiwa pakubwa na kero ya wizi wa mifugo. Akiwahutubia wenyeji wa ol moran, eneo bunge la laikipia magharibi baada ya kukagua miradi ya miundombinu, ikiwemo ujenzi wa barabara ya mahiga kuelekea ol moran na kufungua rasmi majengo ya kituo kipya cha polisi cha ol moran, kindiki amesema vita dhidi ya majangili na wezi wa mifugo imefanikiwa kwa zaidi ya asilimia tisini maeneo ya north rift na kuwataka wananchi kujibiidisha na ukulima, huku akiwaahidi mbolea na mbegu kwa bei ambayo kila mkulima atamudu.

Share: