Kenyans Live

Shirika la ADSOCK kuandaa vikao vya uhamasisho dhidi ya dhuluma za kijinsia

Description (show more)

Shirika la utetezi wa mageuzi ya kijamii, ADSOCK, limeandaa kikao cha majadiliano kitakachohusisha watu wa matabaka mbalimbali katika eneo la Kiserian, kaunti ya Kajiado kuangazia masuala ya usawa wa kijinsia na dhulma za kijinsia. Kikao hicho kinanuia kuelimisha jamii kuhusu mbinu za kushughulikia dhuluma za kijinsia katika jamii zilizotengwa, uwezeshaji kiuchumi wa jamii hizo na kuimarisha uwajibikaji. Shirika hilo linalenga kupanua vikao hivyo katika kaunti nyingine 16 zilizoko kwenye maeneo kame kikiwashirikisha wanaume kwa wanawake kwenye vita dhidi ya dhuluma za kijinsia. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive

Share: