Kenyans Live

Mekanika-2 waaga dunia Naivasha baada ya kugongwa na lori

Description (show more)

Makanika wawili waliaga dunia papo hapo baada ya lori lililokuwa likiendeshwa kwa kasi kupinduka na kuangukia gari aina ya pickup waliyokuwa wakiikarabati katika eneo la Kinungi, Naivasha, kwenye barabara kuu ya Nairobi - Nakuru. Kulingana na wale walioshuhudia kisa hicho lori hilo lililokuwa likiendeshwa kwa kasi likielekea Nakuru kutoka Nairobi, liliondoka barabarani na kuangukia gari hilo upande mwingine wa barabara. Watu wengine wawili waliojeruhiwa walipelekwa kwenye hospitali ya kaunti ndogo ya Naivasha kwa matibabu ya dharura. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive

Share: