Kenyans Live

OCS Lumakanda akamatwa kwa tuhuma za kumdhulumu kingono msichana wa miaka 14

Description (show more)

Ocs wa kituo cha polisi cha Lumakanda amekamatwa kufuatia tuhuma za kumdhulumu kimapenzi msichana wa miaka 14 huko Kikaren, Kaunti ya Kakamega. Wazazi wa msichana huyo wanadai afisa huyo alienda nyumbani kwao wakati wa msako wa pombe haramu na kuwaelekeza wajifiche katika baa iliyokuwa karibu. Wanasema waliporejea muda mfupi baadaye, walimkuta afisa huyo ndani ya nyumba pamoja na binti yao. Familia hiyo inadai kwamba afisa huyo aliwatishia kuwa atawapiga risasi na kisha kuwapa shilingi elfu ishirini ili kumaliza suala hilo. Afisa wa polisi wa Lumakanda amethibitisha kukamatwa kwa afisa huyo, akisema mshukiwa alikamatwa Jumapili jioni na kufikishwa katika mahakama ya Kakamega leo. Polisi pamoja na wawakilishi wa mamlaka ya Ipoa wanaendelea na uchunguzi ili kubaini kilichotokea....

Share: