Kenyans Live

Pukose akosolewa kwa matamshi kuhusu wapiga kura kutoka Uganda

Description (show more)

Mbunge wa Endebess, Robert Pukose, ametoa matamshi ya kutamausha akidai kuwa watu watakaowazuia raia kutoka Uganda wenye vitambulisho vya Kenya kupiga kura watauawa na miili yao kutupwa katika Mto Suam, kaunti ya Trans Nzoia. Matamshi ya Pukose ni ya hivi punde yanayoonekana kuvuka mipaka ya uchochezi na kuzua wasiwasi kuhusu matumizi ya matamshi ya vitisho katika siasa. Na kama anavyoripoti Melita Ole Tenges, Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano (NCIC) imesalia kimya huku kukiwa na madai kwamba imeshindwa kuwachukulia hatua viongozi wanaotoa matamshi ya chuki.

Share: