Kenyans Live

Watu 24 wafariki katika ajali ya Kanga, Mtito Andei

Description (show more)

Watu 24 wamefariki katika ajali ya barabarani eneo la Kanga, Mtito Andei, kwenye barabara kuu ya Mombasa. Miongoni mwa waliofariki ni wachungaji watatu wa kanisa na waumini 21 wa kanisa la Power of the Word International, Kaunti ya Mombasa. Watu wengine zaidi ya 20 wanaendelea kupokea matibabu kutokana na majeraha waliyopata katika ajali hiyo iliyotokea mapema leo. Waumini hao walikuwa wakirejea Pwani kutoka katika mazishi ya mwenzao yaliyofanyika Kaunti ya Kakamega. Maryanne Nyambura anatufungulia jamvi la Nipashe jioni ya leo.

Share: