Kenyans Live

Standard Group yakashifu uvamizi wa ofisi zake na waandamanaji

Description (show more)

Kampuni ya Standard group imekashifu kuvamiwa kwa ofisi zake zilizoko katika barabara ya Nairobi - Mombasa na kundi la waandamanaji waliojitaja kuwa watetezi wa rais William Ruto. Kampuni hiyo imetaja kitendo hicho kuwa ukiukaji mkubwa wa uhuru wa vyombo vya habari na ukandamizaji wa biashara halali. Kundi hilo la waandamanaji lilivamia afisi za Standard group na kuanza kuwarushia matusi wafanyikazi wakidai kuwasilisha waraka wa kuionya kampuni hiyo dhidi ya upeperushaji wa taarifa za kumshambulia rais Ruto

Share: