Kenyans Live

Ruku awaagiza maafisa 84 likizo ya lazima baada ya kashfa ya ulaghai wa mishahara wa KSh bilioni 6.2

Description (show more)

Waziri wa Utumishi wa Umma Geoffrey Ruku amewaagiza maafisa 84 wanaosimamia wafanyakazi wa umma kuchukua likizo ya lazima kufuatia kashfa ya zaidi ya shilingi bilioni 6.2 ya ulaghai wa mishahara. Maafisa hao ni wa Idara ya Magereza, idara mbili za Wizara ya Afya na Idara ya Huduma za Polisi. Ruku anasema hatua hiyo imechukuliwa baada ya ukaguzi wa mishahara ya wafanyakazi katika idara hizo kubaini kulikuwa na hila. Maafisa hao wamepokonywa idhini ya kuingia kwenye mfumo wa malipo ya wafanyakazi.

Share: