Kenyans Live

LSK yataka sheria itake matangazo mubashara ya matokeo ya uchaguzi

Description (show more)

Chama cha Wanasheria nchini LSK, kinaitaka Bunge kuweka wazi katika sheria hitaji la matangazo mubashara ya matokeo ya uchaguzi kutoka vituo vya kupigia kura kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027. Chama hicho kimeonya kuwa kitawakilisha kesi mahakamani iwapo kutakuwa na juhudi za kuzuia uwazi na uwezo wa wananchi kuchunguza matokeo ya uchaguzi. Wanasheria hao pia wameibua wasiwasi kuhusu hali ya utawala na uwajibikaji katika taasisi za umma. Wasiwasi wao unaambatana na onyo kutoka kwa mashirika ya kijamii kuhusu kudorora kwa demokrasia, kuongezeka kwa ghasia za kisiasa na ukiukaji wa haki za binadamu humu nchini.

Share: