Kenyans Live

Ndindi Nyoro aikosoa serikali kwa madai ya wageni kushiriki uchaguzi

Description (show more)

Kinara wa PPK na Mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro, ameikosoa serikali kwa kile anachodai ni kutoshughulikia madai kuhusu kufadhiliwa kwa raia wa mataifa jirani kushiriki katika uchaguzi wa mwaka ujao. Akizungumza katika kaunti ya Meru, ambako alihudhuria ibada ya Jumapili na baadaye kuzungumza na wakazi wa Igembe South, Nyoro amemkosoa Waziri wa Usalama wa Ndani, Kipchumba Murkomen, kwa kile alichodai ni kupuuza suala hilo. Wakati huo huo, Nyoro ametaka mkataba wa makubaliano kati ya serikali na wahadhiri utekelezwe haraka, ili kuzuia kuvurugika kwa masomo katika vyuo vikuu.

Share: