Kindiki amwonya Gachagua kuheshimu wazee wa Mlima Kenya
Description (show more)
Naibu Rais Profesa Kithure Kindiki amemtahadharisha kinara wa DCP, Rigathi Gachagua, dhidi ya kupinga kauli ya wazee wa Mlima Kenya, waliomtawaza kama msemaji wa eneo hilo. Akizungumza alipokagua miradi katika maeneo bunge ya Tharaka na Buuri, kaunti za Tharaka Nithi na Meru, Kindiki amemtaka mtangulizi wake kuheshimu maamuzi ya wazee, akisema wana jukumu la kipekee la kutoa mwelekeo kwa jamii hiyo. Kindiki amesema atatumia nafasi aliyopewa kuendeleza juhudi za kuunganisha jamii za Mlima Kenya na kuhakikisha wakazi wanashirikiana, kuelekea uchaguzi mkuu. Kauli hiyo inajiri huku mjadala kuhusu uongozi na uwakilishi wa kisiasa wa eneo la Mlima Kenya ukiendelea.
Related Videos
More from Citizen TV Kenya
1:11:33
1:47NGERO NA MBAARA CIA ŨKINYANĨRIA WA KIRIU
· 1 views
1:28
2:04Raga | Rising Lionesses waandikisha historia baada ya kushinda medali ya dhahabu
· 1 views
3:41Ruto: Those who can provide internships for young people, we will net off 100% from your taxes
· 1 views
1:28Kenya na Uholanzi zimezindua mipango ya maendeleo
· 1 views
1:44Akenya kũrio mathingate mawatho ma barabara nĩgetha kũnyihanyihia mĩtino
· 3 views
2:04