Kenyans Live

Kenya yapokea tani 11 za vifaa vya kukabiliana na Ebola

Description (show more)

Kenya imepokea tani 11 za vifaa maalumu kutoka India ili kuimarisha maandalizi ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola na dharura nyingine za afya nchini. Msaada huo unawasili huku idadi ya visa vya Ebola vilivyothibitishwa nchini ikifikia wanane kufikia Jumatatu. Watu waliokuwa na mawasiliano na mgonjwa wa kwanza wamewekwa karantini, huku serikali ikisema hakuna maambukizi yaliyoripotiwa katika jamii kufikia sasa. Miongoni mwa walioambukizwa ni wahudumu watatu wa afya. Vifaa vilivyotolewa vinajumuisha mavazi ya kujikinga, vifaa vya maabara na jokofu maalumu kwa ajili ya kuimarisha uwezo wa kukabiliana na mlipuko huo.

Share: