Kenyans Live

Wanafunzi wanane wazuiwa kwa kesi ya mauaji Utumishi

Description (show more)

Wanafunzi wanane wanaohusishwa na mauaji ya wenzao 16 katika Shule ya Upili ya Wasichana ya Utumishi watasalia kizuizini wakati wakikabiliwa na kesi ya mauaji. Jaji wa Mahakama Kuu, Diana Kavedza, amewanyima dhamana, akisema kuwa kuwaachilia kunaweza kuhatarisha maisha yao. Mahakama imeagiza wanafunzi hao kuzuiliwa katika rumande ya watoto ya Kamae Borstal, iliyoko katika Gereza la Kamiti. Uamuzi huo unamaanisha kuwa wanafunzi hao wataendelea kushikiliwa huku kesi dhidi yao ikiendelea mahakamani. Ben Kirui anaripoti.

Share: