Kenyans Live

AFC Leopards yaicharaza Kenya Police FC kwa mabao 2-1

Description (show more)

Klabu ya AFC Leopards imewapa mashabiki wake zawadi ya Siku ya Mashujaa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kenya Police FC katika mechi ya Ligi Kuu ya FKF iliyochezwa Jumanne mchana katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo. Ingwe walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia Kevin Luke Otialo, aliyewahi mpira uliokuwa umepanguliwa na kipa na kuutumbukiza wavuni, na kuipa AFC Leopards bao la kuongoza. Kenya Police FC ilisawazisha kupitia mshambuliaji wa zamani wa Ingwe, Elvis Rupia, na kurejesha ushindani katika mchezo huo. Hata hivyo, Ronald Sichenje aliibuka shujaa wa dakika za lala salama kwa kufunga bao la ushindi na kuipa AFC Leopards ushindi wake wa kwanza msimu huu.

Share: